Ushawahi kutamani kufungua akaunti ya TikTok ya US na ukakwama? Au ushawahi kujaribu kufungua akaunti Mercor, Handshake AI au Alignerr na ukakwama, kisa huna namba ya simu ya Marekani?
Marekani ni moja ya nchi yenye advantage kubwa linapokuja kwenye michongo ya mtandaoni. Platforms nyingi za kufanya kazi mtandaoni huwa zina feature za ziada kwa wakazi wa Marekani na nyingine huenda mbali kwa kuwalipa wakazi wa Marekani pekee.
Platform kama TikTok huwa inawalipa creators wa Marekani kulingana na idadi ya views wanaopata wakazi wa Marekani na pia huwa wana features za ziada kama TikTok Shop kwa wakazi wa Marekani.
Mbali na akaunti za mitandao ya kijamii, platforms za kufanyia kazi mtandaoni hususani kazi za kutrain AI models huwa hazikubali namba za Tanzania wakati wa utoaji wa OTP, hali inayopelekea vijana wengi kukosa fursa ya kufanya kazi na platforms hizo.
Jifunze zaidi: Njia za kupokea malipo ya mtandaoni Tanzania
Kwenye makala hii nitakuelezea kwa undani namna rahisi na ya bei nafuu ya kupata namba ya Marekani kwa ajili ya kuverify OTP kwenye platforms ambazo hazifanyi kazi bongo.
Angalizo: Baadhi ya link kwenye makala hizi ni affiliate na nitalipwa commission kidogo utakapojisajili na huduma hizo kwa kupitia link nilizoziweka hapa.
Mambo ya muhimu kabla hatujaanza
- Ili uweze kutumia kwa amani akaunti yako uliyofungua kwa namba ya US, hakikisha unatumia VPN ambayo location yake inasoma US pia. Baadhi ninazoshauri ni Proton VPN, Nord VPN na Adguard VPN.
- Kuverify akaunti yako haikupi guarantee ya kupata kazi moja kwa moja. Baadhi ya platforms zinazotoa kazi za kutrain AI ni Mercor, Handshake AI, Alignerr, Outlier na Mindrift.
- Njia kuu za malipo kwa hizi platform huwa kupitia Stripe na PayPal ambazo kiuhalisia hazifanyi kazi bongo, lakini unaweza kubypass kwa kuwa na akaunti ya benki ya US kutoka Grey (tumia referral code yangu “Y27DRO” ukiwa unafungua akaunti). Inshort, fanya kazi ulipwe, kufigure out malipo sio kazi ngumu.
- Kwa kazi za kutrain AI, skill pekee inayotakiwa mara nyingi ni uwezo wa kusoma na kuandika Kiingereza. Unaweza tazama interview hii niliyofanya na Emmanuel Mhosole kujifunza zaidi.
Jinsi ya kupata namba ya kuverify platforms za US
Kuna platforms nyingi zinazotoa namba za Marekani kwa ajili ya kuverify OTP. Baadhi ni Quo, Tello na VOIP.
Hizo ni baadhi tu, na binafsi nisingependa kuzungumzia platforms ambazo sijawahi jaribu. Kwenye article hii nitazungumzia platform inayoitwa TextVerified, ambayo nimewahi kutumia kuverify akaunti kwenye platforms mbalimbali.
TextVerified inafanyaje kazi?
Moja ya changamoto kubwa baada ya kununua namba ya Marekani ni pale unaponunua namba kisha uombe OTP na ushindwe kuiona kwenye inbox ya namba uliyonunua.
Kwa TextVerified jambo hilo halikupati, kwani kabla hujaomba namba ya kupokelea OTP wao wanakuuliza kabisa ni platform gani unayotaka kupokelea OTP. Incase hutoiona hiyo platform, maana yake huwezi kuitumia TextVerified kuombea OTP yake.
Kwa maelezo mafupi, TextVerified inakusaidia kupata OTP kwenye platform baadhi, na kwenye kila platform unayoombea OTP lazima ulipie kiasi kidogo ambacho mara nyingi hakifiki hata Tsh 500.