Freelancing na kazi za mtandaoni zinakua kwa kasi sana nchini Tanzania na Afrika Mashariki. Client kutoka nchi za Ulaya pamoja na Marekani wamekuwa wakivutiwa kuajiri wafanyakazi kutoka Tanzania na Afrika Mashariki.

Moja ya njia zinazotumiwa na waajiri hawa ni kuajiri moja kwa moja kupitia mitandao ya kijamii kama LinkedIn na X, pamoja na kutumia majukwaa ya wauza ujuzi kama Upwork, Contra, Fiverr na Guru.

Mbali na uwepo wa wateja wengi wanaovutiwa na wauza ujuzi mtandaoni, bado suala la kupokea malipo kwenye nchi zetu ni changamoto. Kwenye makala hii nitazungumzia njia mbalimbali unazoweza kupokea malipo ukipata mteja wa mtandaoni.

Kwanza, KYC ni nini?

KYC, ama kwa kirefu Know Your Customer, ni njia ambayo makampuni ya malipo yanatumia kuthibitisha taarifa za wateja kabla hawajafungua akaunti kwenye majukwaa yao. Baadhi ya hati zinazoulizwa ni pamoja na:

  • Kitambulisho cha uraia (NIDA)
  • Kitambulisho cha Mzanzibari Mkazi
  • Leseni ya udereva
  • Namba ya TIN
  • Taarifa ya benki ya kuanzia miezi mitatu
  • Kitambulisho cha mpiga kura
Jiunge na Remotika Forum bure. Pata madini kama haya na ujifunze njia za kuingiza kipato mtandaoni pamoja na vijana wengine. Jiunge sasa →

1. Malipo kwenda benki za Marekani

Kampuni nyingi pamoja na wateja wengi wa Ulaya wanapenda kutuma malipo kwenda kwenye akaunti za Marekani kwa kutumia njia maarufu iitwayo ACH. Ukiwa Tanzania kwa sasa kuna njia tatu unazoweza kutengeneza akaunti ya benki ya Marekani yenye ACH: Grey, Wise pamoja na Hurupay.

Binafsi kwa takribani miaka mitatu sasa nimekuwa nikitumia Grey kupokea malipo. Nimefungua akaunti za USD, GBP na EUR. Akaunti ya USD nimeiunganisha na Upwork, ya GBP na Etsy, na ile ya EUR nikipata wateja wa Ulaya huwa nawapa.

Nashauri Grey kwa sababu hizi:

  • Kufungua akaunti ni chini ya dakika 5
  • Huduma kwa wateja iko haraka
  • Wanaruhusu kutoa hela kwa Crypto pia, ambayo mara nyingi huwa na rate nzuri
  • Kadi ya Grey unaweza kuitumia kulipia vitu vya mtandaoni

Ukifungua akaunti Grey unaweza tumia referral code yangu: Y27DRO

Jifunze zaidi: Here is how to get paid on Upwork in Nigeria, Kenya and Tanzania

2. Kulipwa kwa njia ya Wire

Njia hii sishauri sana kutumiwa, kwani makato yake huwa makubwa, na rate wanazokupangia mara nyingi sio nzuri. Makato huanzia $20 hadi $50 na huchukua hadi siku 7 malipo kukufikia. Hela yako inatumwa moja kwa moja kwenda kwenye akaunti yako ya benki ya nchi uliyopo.

Kibongobongo, unaweza kutumia akaunti za benki kama NMB, CRDB na Selcom kupokea malipo yako. Hutakiwi kujisajili na app yeyote, bali benki yako ya nyumbani ndio unatumia. Kupitia njia hii unaweza ulizwa kitu kinaitwa SWIFT code.

3. Kulipwa kwa Payoneer na PayPal

Payoneer na PayPal ni njia zinazopendwa na wateja pamoja na majukwaa mbalimbali. Kwa Tanzania PayPal inasumbua kufungua, unaweza itumia kulipia tu na huwezi kupokelea malipo.

Payoneer pia inasumbua, na huwa sishauri isipokuwa inapokuwa njia pekee. Changamoto kubwa ni makato makubwa, huwezi kutoa chini ya $50, na wanatoza ada ya kila mwaka. Njia ya kukwepa makato ni kuunganisha akaunti yako ya Payoneer na akaunti yako ya Grey ya USD, EUR ama GBP.

4. Kulipwa kwa Cryptocurrency

Hii ni moja ya njia ninazozipenda, ya haraka zaidi na yenye makato madogo. Wateja kutoka nchi zenye vikwazo kama Urusi na China wanapendelea njia hii.

Cryptocurrency ina sarafu nyingi za kupokelea malipo, ila ukiwa mpya nakushauri ufungue akaunti za stablecoin kama USDT na USDC. Hizi huwa na value sawa na USD hivyo ni ngumu kuporomoka kwa haraka. Ukiwa Tanzania nakushauri utumie Binance kufungua wallet yako. Kuwa makini, matapeli wako wengi huku.

Jiunge na Remotika Forum bure. Pata madini kama haya na ujifunze njia za kuingiza kipato mtandaoni pamoja na vijana wengine. Jiunge sasa →