Nimeanza kuingiza hela mtandaoni kupitia kazi za translation mwaka mmoja tu baada ya kumaliza kidato cha sita. Hadi leo naikumbuka hiyo kazi, na uzuri kwenye kupekua pekua nimeikuta kwenye emails zangu.
Andiko hili nitashare hadithi yangu, kwa upande wa kazi za translation pekee. Hakikisha unasoma kila neno, kila nukta, hadi mwisho. Kuna mengi sana utajifunza.
Kazi yangu kubwa hapo ilikuwa kusikiliza audio ya sekunde kadhaa ya Kiingereza kisha nitafsiri kwenda Kiswahili, then nirekodi audio ya yale matamshi kwa Kiswahili. Kitu sikuwa najua ni kwamba huu ulikuwa mwanzo wangu wa kuingiza $10k+ kwa kutafsiri kutoka Kiingereza kuja Kiswahili.
Siku chache zilizofuata nikapata mteja mwingine, na huyu alikuwa na budget ya $300 kwa kazi ya kutafsiri makala mbalimbali. Bahati mbaya aliishia kunilipa $5 pekee, kwani kuna kosa kubwa nililofanya.
Mteja alikuwa analipa kwa kila milestone, na step ya kwanza ilikuwa $5 kwa kila article. Time hiyo nilikuwa busy field, so nikatafuta mtu anifanyie, na uzuri alinifanyia kazi, ila bahati mbaya sikuikagua kabla sijamtumia client.
Client hakuapprove ile kazi, na hapo ndipo nilipishana na $300 yangu ya kwanza ya online. Mwili wangu ulitetemeka sana nikidhani dunia inaisha hapo. Client huyo aliniandikia review mbaya sana, review ambayo hakuna client mwingine angetaka kufanya kazi na mimi. Mind you, hapo nilikuwa na miezi michache tu tangu nimalize kidato cha sita.
Incase unadhani pilika pilika zangu ziliishia hapo, unajidanganya, kwani sikukoma kutafuta fursa za kazi za utafsiri. Safari hii nikasema nazifuata kazi zinapotokea. Moja ya kitu nilifanya ni kuanza kutuma emails kwa agency mbalimbali, nilituma kwa zaidi ya agency 100.
Email yangu ya kwanza nilituma kwenye agency ya UK. Hapo sikuwa na experience, hata jibu nililompa hawakulikubali. Then nikapata client mwingine wa Canada, na akanighost. Imagine experience yako ya kwanza ya kuwa ghosted ni ya client na sio ya mpenzi wako. Nikatuma kwa client wa India, ila sadly project ilikuwa imeisha. Wengine wakaniletea story za assessment kwanza, na kipindi kile ilikuwa ngumu sana kwangu kwani hata lugha ya mkoloni ilikuwa ngumu kuiongea.
But kama maandiko yanavyosema, wakati wangu wa kubarikiwa ukafika, na wateja wakaanza kumiminika. Client wa kwanza akakubali kunilipa, ila pumbavu mimi niliweka nilipwe kidogo, $0.04 kwa neno. Safari ikaenda hadi nikapata wateja wa kunilipa $800+ kwa project.
Ukisoma kwa makini andiko hili utagundua
- Kazi za translation ziko nyingi sana, changamoto ni sehemu za kuzipata.
- Kama hujui namna bora ya kuandika proposal, ni ngumu sana kupata hizi kazi.
Kwa kuligundua hilo, nimeandaa document (database) ambayo ina:
- Agency 100 zinazotoa kazi za translation kwa freelancers (jina la agency na link ya website zao)
- Tools zinazotumika kufanya translation
- Sample email ya kuwatumia watoa kazi za translation
- List ya vendor managers wa LinkedIn na link za profile zao
- Sample proposal za Upwork kwa kazi za translation
Jinsi ya kuipata hiyo document
Kama uko Tanzania unaweza ipata hapa: flutterwave.com/pay/kazizatranslation
Kama uko nje ya Tanzania unaweza ipata hapa: barakamagic.gumroad.com/l/Translationagencies
Hii ni Part 1 tu. Part ya pili nitawaeleza vingi zaidi. Huwa ninasoma comment pia, mnaweza niandikia chochote nami nitawajibu.